CHADEMA YAMLIMA BARUA MCHOME " ATOE MAELEZO NDANI YA SIKU 14"

SALiKi

Administrator
Staff member
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Kilimanjaro kimemuandikia Barua, Lembrus Mchome ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mwanga kwa kosa la utovu wa nidhamu, kufuatia kuhoji kwake uhali wa baadhi ya wajumbe wa kamati Kuu, waliopitishwa na Baraza Kuu ikiwemo Katibu Mkuu wa John Mnyika na Manaibu wake wote wawili.

Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari aliofanya tarehe 24 Machi 2024, Mchome alikili kumuandikia barua msajili, kutokana na kutoridhishwa na majibu ya aliyopewa na katibu Mkuu kwenye barua aliyojibiwa tarehe28 Februari 2025, hayakumridhisha.

Katika barua hiyo Mchome alimtaka msajili kubatilisha maamuzi yote yaliofanyika na kamati kuu, kuanzia tarehe 22 Februari hadi leo, kwa sababu kamati kuu hiyo haikuwa halali, kutokana na baadhi ya wajumbe kutokuwa halali.

Kwenye barua hiyo imemtaka mchome ajitetee ndani ya siku 14, kwa kile kilechoelezwa kuwa kutoa mambo ya ndani ya Chama.
Mchome alikili kupokea barua hiyo, ambayo ilimtaka kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 14.

"Ni kweli nimepokea Barua kutoka kwa Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, wakinituhumu kwa makosa ya kinidhamu, na wametaka nitoe majibu ya utetezi ndani ya siku 14." Alisema Mchome
 
Aiseee!! Huu mwaka wa uchaguzi mbona tuatona mengi, sio kwa CHADEMA pekee, Bali kwa vyama vingine pia ikiwemo CCM.
 
Back
Top